RIPOTI YA SAKATA LA CLOUDS MEDIA YAKAMILIKA

Leo majira ya saa  saba mchana Waziri wa Habari,sanaa,michezo na utamaduni Mh. Moses Nape Nnauye alikabidhiwa ripoti ya sakata la kuvamiwa kwa kituo cha runinga cha clouds tv kilichopo mikocheni jijini  Dar es salaam.

Waziri Nape Nnauye alitoa maelezo macheche juu ya ripoti hiyo kwa kuanza na malalamiko ya kushindwa kumpata Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam licha ya juhudi zao zote za siku mbili kwenda ofisini kwake waliishia patupu.

Mara nyingi walipomuhitaji waliambiwa ana shughuli nyingi za kufanya na siku  waliporuhusiwa kwenda kuonana nae walipofika ofisini hakuwepo na kuhisi kuwa aliwatoroka kwa kupitia njia nyingine na kufanya kushindwa kabisa kupata ushirikiano wake.

Kikubwa ripoti hiyo imeona Mkuu wa mkoa huyo Bw.Paul Makonda amefanya kosa ukiukwaji wa haki za kibinadamu na vyombo vya habari kwa kujiachukulia sheria mikononi na kwenda kuingilia na kulazimisha kufanya vitu ambavyo yeye anataka vikiwa havina ushahidi wa wazi na kuuliza Pande zote mbili.

Pia imeonekana wazi kuwa Mkuu Huyo wa mkoa ameshindwa kutambua ukubwa na ukomo wa madaraka yake  kitu ambacho kimepelekea yeye kujiweka ktk hatari na hata watu wengine kwa kujichukulia sheria miononi.

Amekiuka sheria na maadili ya umma,uongozi wake kama Mkuu wa mkoa kwa kuikandamiza tasnia ya habari.

Vyombo vya habari kwa pamoja vimedhamilia kwa pamoja kutoandika,kuonyesha,kusambaza habari zote zitakazomuhusu mkuu Hugo kwa njia yeyote ile na chombo chochote kitakachokiuka nacho kitaonekana kama adui kwa wanahabari wenziwe.

Kamati imemuagiza Bw .Paul Makonda kuomba msamaha(radhi) kampuni ya clouds media na wafanyakazi wake kwa ujumla kwa makosa aliyowatendea ikiwemo kuwatisha kwa vitendo na kwa maneno kama kuwaambia yeye ana uwezo wa kuwasingizia kesi ya madawa ya kulevya na kuwafunga bila kupitia mahakamani.

Nape aliongeza kuwa yeye sio wa mwisho kwa kutoa maamuzi hivyo nakala ya ripoti hiyo ataipeleka kwa Rais Magufuli,Waziri Mkuu na Makamu wa Rais kwa hatua nyingine zaidi.

Share :

Facebook Twitter Google+ Lintasme

Related Post:

0 Comments "RIPOTI YA SAKATA LA CLOUDS MEDIA YAKAMILIKA"

Back To Top