Majira ya saa nane mchana Mh. Moses Nape Nnauye alikuwa na ahadi ya kukutana na waandishi wa habari ili kuzungumzi kilichomtokea hadi kusababishwa kuvuliwa cheo chake cha uwaziri wa Habari,michezo sanaa na utamaduni leo mapema.Nape aliingia viwanja vya protea hoteli kwa mda aliahidi lakini kabla ya ujio wake eneo ambalo mkutano ulipangwa kufanyika ghafla alitoka mwanamme mmoja kutoka ndani ya hoteli hiyo na kuanza kuwaambia waandishi wa habari waliokusanyika eneo hilo kuwa kwa maagizo kutoka juu mkutano huo sio halali kufanyika na wanatakiwa kutawanyika haraka eneo hilo watafute eneo lingine.
Kauli hii iliwastaajabisha watu walikuwa eneo kwani toka asubuhi mkutano hueo ulipangwa kufanyika eneo hilo na vifaa vyote kuandaliwa ndani ya ukumbi wa hotel hiyo kwa ajili ya ugeni wa waziri aliyetenguliwa bw.Nape. naye Nape ila si hapo.
Alipoingia Nape eneo hilo na alipojaribu kushuka ili kukutana na waandishi wa habari polisi walizuia eneo hilo na kumuamuru asishuke kutoka ndani ya gari hilo na kudiliki kumuonyeshea bastola hata hivyo Nape aliamua kutokeza sehemu ya mwili wake ktk mlango mdogo wa juu na kuanza kuzungumza.
Nape alianza kwa masikitiko na malalamiko kwa vitendo vya uvinjifu wa haki za kibinadamu vilivyofanywa na maafisa usalama kwa kumzuia,kumsukuma na kumtishia maisha,alisema kuhusu kuondolewa ktk cheo hiko yeye kwake kawaida kwani hakumtaka ushauri Rais wakati wa uteuzi wake wala hashangai kumtoa yeye bila taarifa.
Nnauye aliendelea kusema kuwa yeye amefanya alichoamini juu ya waandishi wa habari hivyo hana shida Rais wake Magufuli na anampongez kwa maamuzi yake hayo,Nape alisisitizwa kuwa yeye alikikukuta chama shimoni na kazunguka nchi nzima kufufua cha hadi akapata ajali ya mkono wa kushoto kwa ajili hiyo na kuwafanya watu kushika madaraka leo hii.Yeye ataendelea kuwa mzalendo kwa nchi yake na chama chake daima na ikitokea kufukuzwa chama yeye hana tatizo kwani alishawahi kufukuzwa kabla ya hapo,Nape amewataka vijana kuzungumza ukweli juu ya haki na wala wasiogope chochote.wasikubali mtu mmoja akawa ndio msemaji wa vijana wote,
Nape alifanikiwa kuhutubia akiwa barabarani baada ya kuzuiwa kuingia ndani ya hoteli hiyo ya protea na maafisa usalama walikuwepo eneo hilo.

0 Comments "KILICHOJILI MKUTANO WA NAPE NA WAANDISHI WA HABARI"