
Jina kamili la mwanamziki huyu ni Benard Michael Mnyang'anga aliayezaliwa tarehe 8/septemba 1989 huko makao makuu ya nchi mji wa Dodoma,kwasasa Ben pol ana umri wa miaka 27,Ben pol amezaliwa ktk familia ya watoto wannne kiumjula wao,jina la mama yake mzazi ni Cecilia .
Maisha yake sehemu kubwa amekuwa akiishi jijini Dar es salaam na kusoma shule ya sekondari ya aAzania,kwa makzi ben pol na familia yao wamekuwa wakiishi Vingnguti jijini Dar es salaam.
Ben pol alianza kuimba akiwa na umr wa miaka 17 akiwa sekondari ya azania,Kitu kikubwa ambacho kinamtofautisha Ben pol na wanamuziki wengine wa nyimbo hizi za Taratibu na kimahaba ni Jinsi ya uimbaji wake usiobadilika na wenye kuleta ladha ya kipekee kusikia sauti yake,kutokupitwa na wakati,mwamamziki asiyependa majigambo na kupenda kupaenzi mahali alipozaliwa na asili yao ya dodoma na kupataja na kutumia lugha ya kikwao mara kwa mara ktk nyimbo zake nyingi.
Ben pol amekuwa mwanamuziki aaliyepanda kwa kasi toka kuanza kuimba nyimbo zake rasmi mwaka 2009 na kuanza kuapata mafanikio makubwa kwa kukubalika na watu na kupanda kwa umaarufu wake kwa kila nyimbo aliyoitoa,nyimbo zake nyingi zimekuwa zikishuika nafasi za juu ktk chati mbalimbali za redio,runinga na vyombo vingine vya habari nchini.
Miongoni mwa nyimbo zake maarufu ni kama Nikikupata,pete,jikubali,samboira,maumivu,namba one fan,nakuchana na zile zilizompa umaarufu zaidi za Moyo mashine,Sophia na hii mpya ya Phone aliyemshirikisha Mr.Eazi ambayo inashika nafasi za juu ktk vyombo vya habari.
Bep pol amekuwa akishirikiana na wanamuziki wenzie kama Maua sana,Chid benz,darasa,vj adams,G nako,young dee ktk kazi zao za kimziki.

Ameshapokea tuzo nyingi kwa sifa tofauti ktk aina ya mziki anaoimba ben pol wa R&b,tuzo alianza kupokea mwaka 2011 ktk nyimbo ya Nikikupata kutoka Tuzo za Kilimanjaro awads lakini pia alipokea mwaka 2012 na zaidi ya tuzo nne mwaka 2013.
Ben pol amaekuwa mwanamuziki asiyebadilika mfumo wake wa kuimba(melody) kwa kila nyimbo hivyo kuwa na aina ya kipekee ktk uimbaji wake. Huyu ni mwanamziki chipukizi mwenye mafanikio ktk kazi yake ya mziki wa kizazi kipya (bongo fleva).
Mwanamuziki huyu amekuwa akiishi maisha ya usiri mkubwa nje na mambo ya kimuziki(private life) ila kuna taarifa kuwa Ben pol alizaa mtoto kiume na aliyekuwa mshindani ktk miss Tanzania 2013 Latifa mohamed (Queen Tipha).
0 Comments "BEN POL MFALME WA MZIKI WA R&B NA SOUL ASIYECHUJA WALA KWISHA VIONJO"