VX NERVE AGENT:NI SUMU HATARI ILIYOTUMIKA KUMUUA KIM JONG NAM

Baada ya purukushani yza kurushiana  mpira wa lawama juu ya muhusika wa kifo cha kaka wa mtawala wa korea kaskazini Kim jong un aliyejulikanam kama Kim jong nam aliyekufa ghafla akiwa uwanja wa ndege wa malaysia.

Hisia za mataifa mengi walihusisha kifo hiko kuwa aliyetuma watu kuja kutekeleza mauaji hayo ni mdogo wa Kim jong nam bw, Kim jong un,wataalam wamefanya uchunguzi wa kina juu ya kifao hiko na kugundua kuwa wahusika wakubwa ni Korea kaskazini ila kilichotumika kuua kilikuwa bado hakijafahamika  zaidi ya kuwashukub wanawake wawili na wanaume wanne mabao ni raia wa malaysia na indonesia.

Kufikia leo wataalam wa mambo ya uchunguzi wamegundua kuwa Kim jong nam aliuawa kwa kumwagiwa kemikali ya sumu hatari ijulikanyao kama (Vx nerve agent) sumu hii imekutwa usoni mwa marehemu kim jong nam,sumu hii ni vigumu kuigundua kwa haraka na inaweza kuua papo hapo,dakika au kwa saa kadhaa tu toka kwa mtu kugusa au kumwagiwa hata nje ya ngozi.

Kemikali hii uingia ndani ya mwili na kuharibu mifumo yote ya fahamu na kuifanya kufanya kazi vibaya,,kushindwa kupumua,kuishiwa nguvu kama ilivyo kwa gesi za  sumu za aian ya 9sarin na chlorine) ambazo inaweza kuunguza ngozi,kushindwa kupumua vizuri na kupofua macho.

Mda mchache tu baada ya kumwagiwa usoni sumu hii kim jong nam aliishiwa nguvu na kufa dakika chache tu akiwa ktk clinic ya uwanja wandege wa malaysia,korea kaskazini inashutumiwa kwa kuhusika na mauaji haya na kwa kumiliki kiasi kikubwa  cha sumu za aina hii ya Vx nerve agent ambayo ni hatari sana.





Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "VX NERVE AGENT:NI SUMU HATARI ILIYOTUMIKA KUMUUA KIM JONG NAM"

Back To Top