MAAJABU YA SEKTA YA ELIMU TANZANIA

Kumekuwa na patashika  nguo kuchanika kila pindi ambapo baraza la mitihani tanzania linapotangaza matokeo ya watahiniwa darasa la nne,darasa la saba,kidato,cha nne,sita na vyuo vilivyopo chini ya taasisi hii ya elimu,ukiachana na vyuo vikuu,vyuo vya ufundi ambavyo havisimamiwi na taasisi hii ya elimu.
Kila utakaposikia matokeo yanatangazwa na watoto kufeli mitihani hiyo tuhuma zaidi ya asilia 85% zitaelekezwa kwa walimu wanaofundisha watahiniwa hao.kwa miaka ya hivi karbuni kumekuwa na wimbi kubwa kkt kufeli wanafunzi kitaifa na hasa kwa baadhi ya mikoa kama ilivyotokea mikoa ya mtwara na dar es salaam kwa mwaka 2016-2017 ktk mitihani ya darasa la nne,saba na kidato cha nne hivi karibuni,kufeli huku kulipelekea kushushwa vyeo kwa wakuu wa  shule hizo ikiwa kama adhabu na ovyo kwa shule hizo.
Kwa matokeo haya mabovu ktk nchi hapo ndipo utaziona ofisi husika sasa zinztembelea kwa fujo ktk shule na kutoamaagizo lukuki,kukagua walimu,kuangalia mahudhulio ya walimu,kutaka matokeo ya nyuma ya shule hizo,kushurutisha wakuu wa shule kuongeza mda wa masomo kwa wanafunzi nyakati za jioni na siku za jumamosi ikiwa kama ziada.
Napata tabu sana kwa hali hii kwa kuhisi muda si mrefu walimu wataanza kutiliwa dosari juu ya ubora wa elimu waliokuwa nao ktk ufundishaji na kuonekana kama hawafai na hawajui kufundisha.huko nyuma serikali ya awamu ya tatu ilikuwa na shule nyingi kuliko binafsi na zilikuwa zinazongoza  ktk kila matokeo ya kitaifa shule kama kibaha boys,tabora boys,mzumbe,kilakala,ilbolu,mtwara girls,masasi girls,ndanda sec,songea boys kikubwa asilimia 90% ya shule hizi zilikuwa za bweni.
Idadi ya walimu kwa kipindi hicho ilikuwa haikuwa kubwa sana,vitabu vichache sana kwa ajili ya kujifunzia.
Turudi enzi hizi ambapo serikali imejenga shule za sekondari kwa kila kata na kufanya idadi ya wanfunzi wanafunzi wanaokwenda sekondari kutoka shule za msingi kuongezeka kwa kasi kila mwaka na kumaliza kidato cha nne kwa idadi hiyo kubwa huku nusu yao wakiwa wanafeli kabisa kiasin cha kukosa hata vyeti vya kuhitimu,licha ya idadi ya walimu na vifaa kuwepo kiasi ktk ufundishaji ukilinganisha na hapo zamani. hapo ndipo linapozuka swali gumu kuwa tatizo liko wapi?

SABABU ZA WANAFUNZI KUFELI KTK ENZI ZA SAYANSI NA TEKNOLOGIA
(1)Kutozingatia mitihani ya uchujaji wa wanafunzi kwa darasa la nne,saba,kidato cha pili na kulazimisha kupeleka wanafunzi wasio na uwezo hata wa kusoma neno la kiswahili
.
(2)Shule nyingi kutokuwa na mabweni kwa wanafunzi kuishi eneo la shule ili kuleta ukaribu kwa mwalimu kusimamia mambon yao ya elimu nyakati zote.

(3)Mazingira baina ya ilipo shule na wanapoishi wanafunzi na walimu kuwa mbali kutokana kukosekana kwa nyumba za walimu na mabweni eneo la shuile.

(4)Wazazi na jamii wazazi wamekuwa hawashirkiani na walimu ktk mambo ya elimu hasa pindi wanapokuwa na watorto nyumbani ili kuwaambia wanafunzi kujisomea.

(5)Wanafunzi kutumia vifaa kama simu,kompyuta kwa muda mwingi kwa mambo yasiohusiana na elimu kama facebook,instagram,whatsapp.

(6)Kuondolewa kwa adhabu kwa wanafunzi hii imekuwa tatizo kwa walimu pindi mtoto anapokuwa amekosea jambo inakuwa vigumu kuonya kwa kuohofia serikali na wazazi kwani walimu hupata matatizo makubwa ktk jamii kwa mambo hayo.

(7)Kutokuwepo na mazingira rafiki kwa wanafunzi ktk masomo ikiwemo chakula cha mchana,miundombinu mibovu ikiwepo ofisi,madarasa,vyoo.

(8)Motisha kwa walimu kama kuongeza mishahara ,kul;ipa madeni na stahiki kwa wakati kama pesa za nauli za likizo,usafiri.nyumba za kuishi n.k

(9)Vyama vya wafanyakazi,cwt,tsd kufanya kazi zilizosababishwa kuundwa kwake na si kukaa kimya kama ilivyo sasa juu ya kuongelea maswala ya walimu na elimu na kuwa mifuko ya hifadhi ya jamii ppf,pspf,gepf,nssf,lapf kazi ya kukata pesa tu ktk mishahara na kubaki kimya kila mwezi bila kujua nini kinafanyika wakati wao wako kwa ajili ya maslahi na mambo ya wafanyakazi.

(10)Sekta ya elimu ithaminiwe kama ilivyo ktk bandari,banki kuu,utalii,nishati ambao hupokea mishahara mikubwa na motisha lukuki ikiwepo usafiri,makazi,afya kulipiwa na serikali mda wote wa kazi.

Yako mambo mengi sana yanayosababisha sekta hii ya elimu kudolola siku zote kama kutokuwepo na uzalendo kwa seriklali,kubadili vipimo vya elimu yaani viwango na alama za ufaulu,kubadili na kuanzisha na kufuta masomo hovyohovyo,upungufy wa walimu hasa wa hisabati na sayansi,maabara na vifaa vyake,maktaba zenye vitabu kwa kujisomea eneo la shule,kutosikiliza maoni ya wadau wa elimu,walimu,wazazi licha taasisi kama haki elimu kutoa mambo mbalimbali yanayo iathiri sekta hii.


Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "MAAJABU YA SEKTA YA ELIMU TANZANIA"

Back To Top