"Toka kupata kupambanunikiwa kwa akili ktk ubongo wangu nasikia na kusoma vitabu,majarida,magazeti kuwa Tanzania na Afrika kwa ujumla wake ni miongoni mwa maeneo machache kabisa ktk sayari yetu hii ya dunia kwa kujaaliwa kuwa na rasilimali nyingi na za msingi kabisa ktk kufikia maendeleo ya kweli kama ilivyo kwa wenzetu wa nchi za bara ulaya,marekani na magharibi kwa ujumla wake"
Inasemekana maendeleo tunayoyaona leo ktk nchi za magharibi na marekani ni kuwa waliyachota maendeleo hayo kutoka barani afrika nyakati zile za ukoloni ktk karne 18 na 19,wazungu walitawala afrika na asia kwa nguvu zote na kuchota mali nyingi sana walizokwenda kwao na kuwatajirisha wananchi wa huko na kuwapa nafasi ya sasa waliyonayo ya nguvu za kiuchumi,kijeshi,kijamii,kiteknolojia n.k
Swali langu linabaki kichwani kila siku ni kuwa "Kwanini sasa wenye mali hizi ambazo hadi sasa zipo na tunazo tunazmiliki utawala wetu binafsi toka kupatikana kwa uhuru au kuondoka kwa wakoloni hao bado hazitunufaishi?
Kila kukicha watu wetu
wanaendelea kuogelea ktk tope zito la umasikini uliokithiri,watu wanashindwa hata kupata njia za kupata chakula chao binafsi cha kila siku,watu wanashindwa kununua mavazi yao,kuwa na makaazi mazuri,uwezo wa kupata matibabu n.k
''Najiuliza je wakoloni bado wako ktk ardhi zetu wakiendelea kujinufaisha na rasilimali zetu za madini,ardhi,misitu,bahari,gesi,mafuta,wanyama na wakituacha wenyeji hatuna cha kupata nyuma yake?
Na kama ni hivyo ni nani huyo ambaye anaruhusu tena hali hii mbaya ya ukoloni kurudi tena barani afrika au Tanzania?
Na kama si hivyo kuwa wakoloni hawapo je ni kipi hicho tena kinachotusumbua waafrika au watanzania au kutuwekea vikwazo ktk kufikia kilele cha maendeleo ya kisasa kama china,marekani na ulaya baada ya nusu karne ya kuachwa huru na wakoloni hao?
Nitajaribu kugusia sababu chache kabisa zinazoendelea kututesa,kututafuna,kutururudisha nyuma waafrika au watanzania:-
SIASA NA TAWALA-
Hii ni miongoni mwa sababu kubwa kabisa barani afrika ktk kuchangia asilimia zaidi ya 70% ktk kuendelea kiuchumi,Tamaa za madaraka,aina za tawala kama za kidemokrasia,udikteta,ujamaa zimekuwa zikivuruga maendeleo ya kweli na kuleta machafuko ya kisiasa ya watu wa nchi hizo kama ilivyo sasa Sudani Kusini,Somalia,Msumbiji,Nigeria na Congo DRC,tawala hizi zinakaa madarakani kwa maslahi ya mataifa mengine hasa ya ulaya.
KUSHINDWA KUSIMAMIA SHERIA NA SERA KWA MAKUSUDI-
Kwa makusudio kabisa baadhi ya viongozi waliopo na walipewa mamlaka mbalimbali na wananchi aua watawala wa juu uamua kukwamisha mambo mengi ya kisheria kwa makusudi au kwa kutaka kujinufaisha wao binafsi na kaucha kundi kubwa la wananchi likiteseka,na hata inapotokea waziwazi aliyepewa mamlaka amefanya kosa vyombo vya usalama vinasshindwa kufanya kazi yake kwa kuhofia mammlaka ya kundi hilo,hali hii usababisha kuendelea kwa ukikwaji wa haki za kibinadamu na kushindwa kuwa kutekelezwa kwa mambo mengi yaliyokubalika kisheria au kisera.
KUTOKUWEPO KWA NISHATI YA UHAKIKA NA INAYOJITOSHELEZA NCHINI (UMEME)-
Ikiwa umeme wa jua,nyuklia,upepo,maji yote sawa ilimradi nishati hiyo iwe ya uhakika na yenye kujitosheleza ktk kuendesha shughuli za viwanda vikubwa,vidogo na hata vya kati,Swala la nishati ya uhakika imekuwa tatizo kubwa nchini kwetu na imeshakuwa ni kidonda kisichopona licha licha ya kuwa na vyanzo vingi vya kupatia nishati hizo ikiwemo ugunduzi wa gesi ktk mikoa ya kusini na maeneo mengine,hili ni tatizo kubwa ktk kurudisha nchi na mtu mmoja mmoja kimaendeleo au kiuchumi,umeme ni uti wa mgongo ktk taifa kuendelea kiviwanda na hata kijamii
.
Tatizo hili limekuwa sugu kabisa kutokana na kushindwa kwa kutekelezeka kwa makubaliano na mikakati ya sekta hiyo,wananchi wengi bado hawajafikiwa na nishati hii na hata wale waliofikiwa bado imekuwa si a uhakika kabisa,nishai a umeme imekuwa ni jambo la msingi kabisa kwa maaifa yalioendelea.
KUSHINDWA KUWEKEZA KTK MIUNDOMBINU-
Barabara,reli,viwanja vya ndege,Bandari ni mambo a msingi sana kwa taifa lolote kuendelea mbele,kutoa wau au mizigo sehemu moja kwenda mahali kwengine uegemea sana kuwepo kwa vmiundombinu ya uhakika ena inayopitika nyakati zote ya majira ya mwaka,Barabara na maeneo mengi barani afrika zimekuwa hazipitika wala kufikika kwa urahisi zaidi kutokana na hali ya kukosa miundombinu ya uhakika au kutokuwepo kabisa.
KUSHINDIKANA KWA MAPINDUZI YA KWELI YA KILIMO NA UFUGAJI-
Kilimo na ufugaji ktk nchi za kwetu za kiafrika imekuwa ni sehemu ya kuleta migogoro na mapigano makubwa bana ya wakulima na wafugaji licha ya kuwa na sehemu kubwa ya ardhi inayofaa kwa kilimo na ufugaji,uingereza,India,USA,China na Mataifa mengi ya ulaya yalitambua umuhimu mkubwa wa kilimo na ufugaji ktk kupiga hatua ktk kufikia maendeleo ya kijamii na kiviwanda,viwanda vingi vinategemea malighafi kutoka ktk sekta ya kilimo na ufugaji ukiachana na viwanda kama vya Chuma,hivyo hakuna viwanda bila kuendeleza kwanza kilimo na ufugaji,viwanda vingi vilivyoanzishwa nyakati za utawala wa awamu ya kwanza vilikufa mwanzoni mwa miaka ya 1990 kwa kukosa malighafi na nishati ya uhakika.
KUDHARAULIKA KWA ELIMU YA KUJITEGEMEA-
Si ajabu kabisa kwa mhitimu wa chuo kikuu wa shahada au stashahada Uhandisi kushindwa hata kubadilisha taa iliyoungua chumbani mwake na badala yake kumwita mtu wa darasa la saba kuja kuifanya kazi hiyo,Tatizo hili linasababishwa na kupotezwa kwa elimu ya kujitegemea ambayo Hayati Baba wa Taifa aliisisitiza ktk Azimio la Arusha la 1967,Elimu ya kujitegemea ndio msingi mzuri kwa mwanafunzi kuweza kujiajili pindi amazilizapo masomo yake,Vituo vyetu vya elimu vimekuwa vichache na havijitoshelezi kwa vifaa na hata walimu ktk ufundishaji.
KUTOKUWEPO KWA MIPANGO MIKUU YA KITAIFA ISIYOBADILISHWA NA TAWALA-
Marekani ni miongoni mwa nchi ambazo kiongozi atakaa mdarakani kwa ajili ya kuwaongoza wanachi ktk kutekeleza mipango iliyokubalika ktk kuendeleza taifa na si vyenginevyo,Mipango ya kitaifa upangwa na baraza la Congress na sio kiongozi wala chama,hii ni tofauti na barani afrika kwani mambo ya kitaifa ubakia mikononi mwa watawala na sio kama yaliyokubaliana ktk bunge au vikao vya wataalam.
KUWEKA SIASA,UDINI,UKABILA,CHAMA,UJIMBO MBELE KULIKO MASLAHI YA KITAIFA-
Hali hii wenzetu walishaitoka miaka zaidi ya 300 iliyopita kwani waligundua inawarudisha nyuma kwa kiwango kikubwa,makundi haya serikali ilipambana nayo kwa nguvu zote kuhakiksha yakufa au kupotea kabisa vichwani mwa raia zao,kikubwa walipandikiza mbegu ya uzalendo kwa ajili ya maslahi a kitaifa,hii ni tofauti na barani afrika ambako tabia hizi ndio zimetapakaa kwa kiasi kikubwa.
KUKITHIRI KWA RUSHWA NA KUKOSA ELIMU KWA RAIA WENGI-
Wengi ktk raia kutoka barani afrika hawajui kusoma wala kuandika hili ni tatizo kubwa sana ktk kuwapeleka wananchi ktk maendeleo ya kweli,elimu ndio msingi wa mambo yote,hivyo nchi inayotaka maendeleo ya kweli ni lazima kuhakikisha wananchi wake wanapata elimu ya kujitambua na kujitegemea kwa maslahi ya nchi zao.
Tunapoazimisha miaka 18 taka kututoka kwa Muasisi na Kiongozi wa kwanza wa Taifa hili la Tanzania Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Mnamo siku ya alhamisi Oktoba 14 1999 akiwa na umri wa iaka 77 ni lazima tusimamie yale ambayo yalionekana wazi kuwa yalitoa mwangaza wa maendeleo kwa taifa hili,Nyerere alionyesha bidii kubwa ktk kuijenga nchi hii kwani hata idadi kubwa ya viwanda vilijengwa nyakati za utawala wake na vilifanya kazi vizuri sana kabla ya kuja kufa ktk miaka ya 1990 baada ya kuuacha ujamaa na kukumbatia ubepari ambao mpaka sasa tunalia nao kwa jinsi unavyotunyonya wananchi na nchi yenyewe kwa rasilimali zetu kuendelea kusafirishwa.
Lazima tubadilike nyoyoni mwetu na ktk matendo ili kufikia maendeleo ya kweli,China kwa sasa ina majiji zaidi ya 14 makubwa yenye wakaazi wasiopungua milioni 6 na kuendelea kila moja,hali ya majiji haya ktk miundombinu,usafi,uchumi yako vizuri na yanapendeza zaidi,tuige mfano huu au ukitushndwa huo tuangalie hata korea kaskazini licha ya wao kubanwa kiuchumi na tawala za dunia ya tatu.

0 Comments "TUNATELEZA WAPI KUFIKIA MAENDELEO YA KWELI TANZANIA!!!!"