MAELFU WAANDAMANA KUTAKA JIMBO LA CATALONIA KUPATA UHURU

Kwa miaka kadhaa sasa raia wa jimbo la Catalonia lililopo kaskazini mashariki mwa nchi ya Uhispania wamekuwa wakiomba kupiga kura ya maoni  kwa serikali ya nchi hiyo juu ya kujiondoa kutoka mikononi mwa uhispania bila mafanikio yeyote yale,Mwaka huu 2017 umekuwa mwaka wa vujo na visa zaidi kuwahi kushuhudiwa kwa kile kinachoendelea baada ya maelfu ya raia kumiminika barabarani huku wakiwa wamebeba mabango makubwa na bendera za kutaka uhuru wao ktk jimbo hilo.

Hii imekua kawaida kwa sasa duniani kwani kwa sasa Iraq jimbo la Kirkuk nalo liko mbioni kutaka kupiga kura za maon ili kujetenga na serikali ya iraq,Jimbo hili kwa asilimia kubwa linakaliwa na wairaki wenye asili ya Kikurdi ambao toka enzi za utawala wa Saddam Hussein wamekuwa wakipinga kuwepo ndani ya iraq.




Hali hii imeshashuhudiwa huko nyuma kwa kujitenga kwa jimbo la Kosovo kutoka Serbia,Crimea kutoka nchi ya Ukraine,Sudan kusini kutoka Sudan baada ya migogoro ya mda mrefu ktk nchi hizo ikiwemo ya kikabila,kisiasa,utawala,kidini,Kugombea rasilimali mbalimbali kama Mafuta,gesi,Madini n,k





Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "MAELFU WAANDAMANA KUTAKA JIMBO LA CATALONIA KUPATA UHURU"

Back To Top