
Ajabu kubwa ktk eneo hili ni juu ya bahari yake iliyozunguka kisiwa hiko,Eneo linalojulikana kama
(Bermuda Triangle au Devil's triangle) ndio eneo hatari kabisa na linaloogopwa hasa na wanaotumia bahari na hata anga la eneo hilo kwani ni eneo hatari kabisa kuwahi kuwepo ktk bahari zote tano yaani ile ya Pasifiki,atlantiki,Hindi bahari ya kusini na ile ya aktiki kaskazini kwa dunia!
Makumi kwa mamia ya meli,ndege,watu Wengi sana wamepotea bila kujulikana wapi na kipi kiliwapata kabla kufa au kupotea na vyombo vyao hivyo bila kupatikana ushahidi wa mabaki ya vyombo vyao walivyokuwa wakisafiria.

Ikumbukwe kuwa zaidi ya asilimi 71% ya dunia nzima ni kusanyiko la maji tu na 29% pekee ndio ardhi tunayoishi.
Mabaharia Wengi wanakubali kuwa eneo la bahari ndio eneo lenye maajabu mengi zaidi yasiyofahamika wala kuwa na maelezo ya kina kuliko angani au nchi kavu.

Ndio eneo linalokaririwa kuzamisha meli nyingi zaidi kubwa na ndogo kuliko eneo lolote lile,vyombo vinapofika mahali hapa ujikuta vinakosa Nguvu na kupoteza mwelekeo ghafla na kuzama.
Ikumbukwe hata meli ya TITANIC iliyokuwa ikitokea jiji la Southampton uingereza ikielekea jiji la New York marekani iliyobeba watu wapatao 2224 na kuua watu 1500 mwaka 15/4/1912 ilizama eneo la jirani kabisa baada ya kugonga Barafu kubwa iliyokuwa ikielea baharini ktk sehemu hii inayoaminika kuwa ya kishetani.
0 Comments "BERMUDA DEVIL'S TRIANGLE! (ENEO LA GHARIKA NA MAUAJI DUNIANI!)"