MUGABE AMKEJELI TRUMP HADHARANI

Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe amekejeli Rais wa Marekani Trrump ktk hotuba yake ndefu aliyoitoa ktk mkutano huo wa 72 toka kuanzishwa kwake 1945 baada ya kwisha kwa vita kuu ya pili ya dunia.

Mugabe amemwita Trump kuwa yeye ni sawa na Ujio wa mara ya pili wa Goliati ktk ulimwengu kwa maneno yake makali na ya vitisho anayoyatoa kwa nchi za Iran,Korea Kaskazini,Palestina,iraq,syria kwa kuendeleza kuzichafua nchi hizo kwa vita na migogoro ktk maeneo hayo.

Trump amekuwa mgumu ktk kuunga mkono juu ya kuapambana na mabadiliko ya hali ya hewa na kukaa pembeni kabisa,Mugabe amemwambia Trump kuwa sasa sio mda wa vitisho na majigambo kwa wenziwe bali ni mda wa kukubaliana na hali halisi ya maisha ilivyo ktk hali ya hewa na amani kwa dunia.

Mugabe amemwita Trump kuwa ni kama Goliati anayetaka kukandamiza haki za kibinadamu kwa kutumia mabavu yake ya kijeshi,kiteknologia,kiuchumi ili kuogofya nchi nyingine juu yake,Mugabe aliongeza kuwa Trump ajitahidi kupuliza Tarumbeta (Trumpet) lake zaidi kwa kutetea amani na usalama wa wanadamu na si kuondoa maisha ya watu au kuharibu mazingira ya dunia.
Hivi karibuni Vimbunga Harvey na Maria vimepiga na kuahribu vibaya nchi za Haiti,Cuba,Dominican republic,Porto rico ikiwa ni athari za mabadiliko ya hali ya hewa hayo hayo.

Itakumbukwa kuwa Rais Mugabe sio mara ya kwanza kubeza nchi ya marekani na bara ulaya ktk mambo mengi ya uonevu unaofanywa kwa mataifa ya afrika na asia hasa kupitia baraza la usalama la umoja wa mataifa (UN) kwa kura ya veto inayopigwa na mataifa machache tu yenye nguvu(Marekani,ufaransa,ujerumani,uingereza,urusi)

Mugabe aliongea kwa kumagiza Katibu wa umoja wa mataifa wa nyakati hizo ndugu Ban Ki moon kuwa aende kuwaambia umoja wa ulaya,marekani wanyamaze kabisa kwa kufunga midomo yao juu ya kuzisakama nchi za kiafrika ktk swala la kidemokrasia kwakuwa hata wao wa ulaya ndio watu wa kwanza kuharibu na kukandamiza misingi hiyo ya kidemokrasia wanayo hubiri kila kukicha kwa kualazimisha nchi nyingine kuacha mila na desturi zao kwa kutaka kukubali mila zao za magharibi za ushoga.

Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "MUGABE AMKEJELI TRUMP HADHARANI"

Back To Top