TAARIFA ZA UCHUNGUZI ZA AL-JAZEERA ZAWAPONZA KUFUNGIWA OFISI ZAO ISRAEL

Mtandao mkubwa wa habari duniani wa Al-jazeera makao makuu yake nchini Qatar ktk jiji la Doha umejikuta matatani tena kwa kuendelea kubanwa na taifa la israel kwa kuwataka kuwafungia ofisi zao zilizopo mjini jerusalem Israel.

Waziri mkuu wa israel Benjamin Netanyau amekaririwa akisema kuwa wako mbioni kufanya taratibu za kuifungia mitandao hiyo ya habri ya al jazeera inayofanya kazi zake nchini humo kwa kuwa wao pia wana shaka na shutuma zilizotolewa na matifa kadhaa kuwa chombo hiko cha habari kinajihusisha na mambo ya kusaidia vikundi vya kigaidi,kuwapa hifadhi,kusaidia kifedha.

Al jazeera ambao kwa kawaida uibua taarifa nyingi za msingi zilizojificha ktk mataifa mbalimbali hasa ktk maeneo ya kivita,njaa,magonjwa,rushwa,umasikini,haki za kibinadamu wanajikuta mara kwa mara wakiingia ktk migogoro na nchi husika kwa kutoa taarifa ambazo tawala husika huwa hawataki zijulikane na jumuiya za kimataifa.

Miongoni mwa masharti waliyopewa nchi ya Qatar na nchi majirani wenzake kama Saudi arabia,Jordan,UAE ni kuacha kushirikiana na vikundi vya kigaidi kama vya Hizbuallah,Al qaeda,Taliban,Gaza pamoja na kuifungia mitandao ya habri ya aljazeera.


Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "TAARIFA ZA UCHUNGUZI ZA AL-JAZEERA ZAWAPONZA KUFUNGIWA OFISI ZAO ISRAEL"

Back To Top