UNATAMBUA NINI KUHUSU NYANGUMI NA MAISHA YAKE

Blue whale! Nyangumi wa bluu ndiye kiumbe mkubwa zaidi duniani mwenye uzito wa kilo laki mbili (200,000) sawa na tani 200.

Mnyama huyu wa baharini kwa Siku anakula chakula chenye uzito wa kilo 3600 Sawa na tani 3.6

Moyo wake pekee una uzito wa kilo 250 sawa na uzito wa watu wanne 4,kila mmoja akiwa na uzito wa kilo 62..!

Wanyama hawa wa baharini wenye maumbile makubwa kabisa wako wa aina nyingi Ila huyu blue whale ndio mkubwa zaidi mwenye urefu wa mita 30.

Tambua kuwa kuna aina zaidi ya 86 za wanyama hawa nyangumi lakini aina hii ya Blue whales ndio wenye maumbile makubwa zaidi kuliko aina zote zilizobakia.

Killer whales ni aina ya nyangumi wenye maumbile ya kawaida ila sio yao kubwa wao wanaogelea kwa kasi kubwa pia wanasifika kwa kuwinda na kuua aina nyingi za samaki na hata papa.

Aina hii ya nyangumi utembea kwa makundi makubwa na uishi kwa kuhamahama.




killer whale au nyangumi wauaji

Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "UNATAMBUA NINI KUHUSU NYANGUMI NA MAISHA YAKE"

Back To Top