ROLLS ROYCE YAZINDUA GARI YA KIFAHARI YENYE THAMANI YA BILIONI MOJA.

Kampuni kongwe ya Rolls royce ya nchini uingereza inayotengeneza magari yake ya kifahari yanayotumiwa na watu maarufu kama,viongozi,wanamuziki na waigizaji,wanamichezo na matajiri wengi duniani kutokana na ubora wake wamezinduagari mpya kwa mwaka huu wa 2017 ya ROLLS ROYCE PHANTOM VIII.

Gari hii ya kifahari kabisa kuzinduliwa toka kuanzishwa kwa kampuni hii mwaka 1925 itagharimu zaidi ya dola milioni mia nne na arobaini elfu (440,000) au sawa na Euro 375,000 ikiwa ni sawa na pesa za kitanzania milioni mia tisa na sitini na elfu (968,000,000).

Rolls royce ni miongoni mwa gari zinazozalishwa kutoka kampuni kongwe ya British motors works (BMW) ikiwa ni kampuni inayosifika kwa kutengeneza gari imara na bora zaidi duniani na kufanya kuwavutia watu wengi wenye uwezo mkubwa kumiliki gari hizi licha ya bei zake kuwa za gharama za juu sana.


Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "ROLLS ROYCE YAZINDUA GARI YA KIFAHARI YENYE THAMANI YA BILIONI MOJA."

Back To Top