MAGUFULI ACHARUKA:MWANAFUNZI ATAKAYEPATA MIMBA AKIWA SHULE ASAHAU KUHUSU MASOMO

Rais John Pombe Magufuli amewajua juu wanafunzi wazazi na mashirika yasiyo ya kiserikali yanayotetea haki ya wanafunzi wa kike wanapopata mimba wakiwa ktk masomo hasa kuanzia elimu ya msingi hadi sekondari kuwa waruhusiwe kuendelea na masomo pindi tu watakapojifungua ili kuepeuka kuwanyima haki yao ya kupata elimu kwa kosa hilo.

Kwa kipindi kirefu sasa mashirika hayo yasiyo ya kiserikali yamekuwa yakipiga debe juu ya kuendelea na masomo kwa wanafunzi wa kike hata wanapopata mimba wakiwa shuleni kwani wengi wao wamekuwa wakirubuniwa au kubakwa na watu wasio waaminifu a waliokosa maadili hivyo inakuwa ngumun kuhukumu kuwa walifanya makusudi.

Wimbi kubwa la watoto wakike wamejikuta wakishindwa kuendelea na masomo hasa ktk miaka ya hivi karibuni kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo hii ya kupata mimba wakiwa masomoni hivyokuwalazimu kukatisha ndoto zao hizo papohapo kwa kufukuzwa shule.

Rai hii imegonga mwamba jana pale Rais Magufuli alipoitolea ufafanuzi wa wazi ktk mkutano wake wa uzinduzi wa barabara ya Bagamoyo Masata kwa kuwaambia kuwa jambo hilo ktk utawala wake kamwe halitowezekana kwani serikali haipo kwa ajili ya kusomesha wazazi bali wanafunzi tu,mwanafunzi yeyote atakayeamua kubeba mimba huku akijua wazi yeye mwanafunzi na hatakiwi kufanya hivyo basi aelewe wazi kuwa atakuwa amejifukuzisha shule yeye mwenyewe na kamwe hatoruhusiwa kuendelea na masomo.

Amesema kuwa 'mashirika haya yanayojifanya kutetea haki za wanafunzi sijui kama wao nao walibeba mimba wakiwa masomoni au la'

Hii ni kukiuka mila na maadili ya nchi kwani kuruhusu jambo kama hilo ni sawa na kituko tu na kutawafanya wafunzi wote kufanya jambo hilo  bila uoga wala aibu yeyote ile kwani wakijua hakuna kitakachowakuta kama adhabu kwao.

Serikali iliamua kuania mwaka 2016 wanafunzi kuazia shule za msingi na sekondari kidato cha nne watasomeshwa kwa gharama za serikali ambazo mpaka sasa kila mwezi utoa zaidi ya shilingi bilioni 18.77 kama gharama za shule zote. kwa ajili ya wanafunzi hao ktk nchi nzima.




Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "MAGUFULI ACHARUKA:MWANAFUNZI ATAKAYEPATA MIMBA AKIWA SHULE ASAHAU KUHUSU MASOMO"

Back To Top