Kufikia sasa ulimwenguni kuna aina nyingi za usafiri yaani ule wa kiasili na mkongwe kabisa wa kutumia miguu,Barabara,wa majini,reli,wa majini na ule wa angani. Ktk aina zote hizi za usafiri zina mazuri na matatizo yake kutegemeana na mtumiaji.
Usafiri wa anga ndio usafiri pekee wa haraka na unaoweza kumuwezesha mtu kusafiri kwa umbali mrefu zaidi ikiwa kutoka bara moja hadi lingine au kutoka sayari moja hadi nyingine kwa kutumia mda mchache tu.
Licha ya uzuri wa usafiri huu kuwa ni wa haraka zaidi,unaoweza kumpeleka mtu au mizigo kwa umbalimrefu zaidi,usio na ajali za mara kwa mara ukilinganisha na usafiri wa barabara ,reli au majini bado usafiri huu unakuwa ndio usafiri hatari zaidi pale pindi inapotokea makosa au hitilafu yeyote ya kiufundi wakati ndege inapokuwa angani inaweza kutokea ajali ambayo kuepuka kwake kunakuwa kwa asilimia chache sana na hata kama kupona au kunusurika kwa watu,mizigo na chombo chenyewe kunakuwa sawa na asilimia 10% tu.
Baadhi ya mambo ambayo yanaweza kusababisha ajali ya usafiri wa anga ni kama yafuatayo:-
Makosa ya kiufundi au hitilafu za kimitambo za chombo husika-
Kufeli au kushindwa kufanya kazi kwa moja au baadhi ya chombo au vyombo vya nduge inapokuwa angani kunaweza kuchangia kwa asilimia kubwa ktk kupata ajali kwa ndege hiyo.
Makosa ya kibinadamu ambayo uyanaweza kufanywa na waongoza ndege walio ktk vituo-
Kumekuwa na wimbi kubwa ajali za ndege ktk nyakati mbalimbali ambazo vyanzoi vyake uwa ni makosa ya waongoza ndege hizo ambao wanakuwa ktk vituo mbalimbali duniani (Control centre) wamekuwa wakishindwa kuwasiliana ipasavyo na madereva wa ndege pini zinapokuwa angani hivyo kusababisha ndege hzo kuanguka,kugongana zenyewe kwa zenyewe.
Makosa ya madereva wa ndege (Pilot errors)-
Wakati mwingine madereva wa ndege hasa kubwa kwa kawaida wanatakaiwa kuwa wawili wanaweza wakijikuta wakisababisha ajali kutokana na kutokuwa makini na kuongoza ndege ktk kusoma na kutafsiri ishara na milio mbalimbali inayotolwa na ndege ktk ubao uliuo mbele yake (Dashboard)
Ishara na milio itolewayo na ndege uwa na maana kubwa sana hasa ya kumuonyesha dereva juu ya tatizo lilipo ndani ya ndege yake hiyo,kama kuisha kwa mafuta,kupasuka kwa mitungi ya gesi,kufeli kwa injini au kifaa chochote nje ya ndege yake.
Baadhi ya madereva wa ndege hizo wamejikuta wakiidharau miito na ishara hizo na kuendelea na safari kwani wakati mwingine kwa bahati mbaya miiti na ishara hizo ujitokeza na kulia bila kuwepo kosa au hitilafu yeyote ile.
Hali ya hewa au mabadiliko ya anga kwa ghafla-
Kulipika kwa milima ya kivolkano ambayo huasili kwa kiasi kikubwa utendaji kazi wa injini za ndege na wakati fulani kusababisha injini na mifumo mingine kushindwa kabisa kufanya kazi kwa vifaa.
Kuwepo kwa radi kali ambazo wakati mwingine upiga ndege licha ya kuwepo kwa kifaa maalum cha kuzuia hali hiyo,hali hii usababisha hatari ya kutokea moto ktk ndege.
Kuvamiwa na watekaji nyara wa angani (Hijacking or Hijackers)-
Kutokana na kushuka kwa kiwango cha usalama wa dunia kumekuwepo na tabia ya baadhi ya watu au vikundi va kigaidi kuingia ndani ya ndege na kuisuburi inapokuwa angani kuanza kuiteka ndege na kuingoza ndege kwa kuwapa amri madereva wa ndege kuipeleka wanavyotaka wao ikiwemo kutishia kuilipua ndege au kupiga risasi kitu ambacho ni hatari sana kwa usalama wa watu walio ndani ya ndege.
Kutofanyiwa kwa matengenezo ya mara kwa mara (Services)-
Makosa yanayofanywa na wanadamu wenyewe ya kutokuwa makini ktk kufanyia marekebisho na kutazama chombo husika mara kwa mara pia inaweza kuwa moja ya sababu ya ndege kupata ajali hasa inapokuwa angani kwani makosa kama ya kutokufunguka kwa milango ya kutolea matairi kwa ajili kutua ndege,makosa ya kutofunga milango kwa makini na kusababisha kufunguka pindi inapokuwa angani.
Licha ya kuwepo kwa hatari hizo za usafiri huo wa anga bado ndege na aina hii ya usafiri inabaki kuwa ndio usafiri salama na wa haraka zaidi dunia kuliko aina nyingine zote zilizopo.
Usafiri huu ulivimbuliwa kwa mara ya kwanza na kundi la ndugu wa WRIGHT BROTHERS kuanzia miaka ya 1903 licha ya harakati zake kuanza toka mwaka 1899 na kundi hilo
0 Comments "FAHAMU SIRI CHACHE ZA USALAMA,HATARI ZA USAFIRI WA ANGANI (NDEGE)"