UINGEREZA SASA HAPAKALIKI:SHAMBULIZI LA KIGAIDI LATOA UHAI 22

Zaidi ya watu 22 wamefariki dunia papo hapo na 60 kuumia vibaya ktk shambulizi la kigaidi la kujitolea muhanga huko uingereza ktk mji wa Manchester kwenye uwanja mkubwa wa (Manchester Arena) kulipokuwa kunafanyika onyesho la mziki la mwanamuziki kutoka nchini marekani ajulikanaye kama Ariana Grande ambalo limefanyika jana usiku mei 22 2017.

Tamasha hilo lilifanikiwa kuchukua watu wengi waliohudhuria ktk uwanja huo mkubwa wenye uwezo wa kuchukua zaidi ya watu 2,1000 uliofunguliwa july 15 1995,shambulizi hili linalohisiwa kufaywa na mshambuliaji wa kiume alipandikiza mabomu ya kujitengenezea mwenyewe lilitokea saa nne usiku kwa majira ya uingereza.

Hali ya majeruhi 8 waliopo hospitali imekuwa mbaya zaidi na kuwafanya watu kuhofia idadi ya vifo kuongezeka zaidi.

Zaidi ya simu za dharura 240 zilipigwa usiku huo,gari za kubeba wagonjwa 60 zilifika eneo la tukio na polisi zaidi ya 400 walikuwepo sehemu hiyo kusaidia majeruhi.

Polisi wanaendelea na uchunguzi wa gaidi huyo kujua kama ana mafungamano na kundi lolote la kigaidi au ni mwenyewe. Uingereza imekuwa ikikumbwa na mashambulizi haya ya kigaidi mara kwa mara hasa ktk makundi ya watu.









Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "UINGEREZA SASA HAPAKALIKI:SHAMBULIZI LA KIGAIDI LATOA UHAI 22"

Back To Top