
Mkuu wa mkoa kilimanjaro ndugu Saidi meck Sadiki na majaji wawili wa mahakama kuu Bwana Aloysius Kibuuka Mulizi aliyekuwa jaji wa mahakama kuu tanzania na mwenyekiti wa tume ya kurekebisha sheria Tanzania,Bi Upendo hillary Msuya aliyekuwa jaji wa mahakama kuu Tanzania, wote kwa pamoja waliomba kuacha kazi kwa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania mh. John Pombe Magufuli.

Raisi amaridhia maombi yao wote kwa pamoja na kuwaachisha kazi siku ya tarehe 15 mei 2017 na taarifa kutolewa mei 16 2017.
Bado hakuna taarifa rasmi ni kwanini au kwasababu zipi zilizowafanya mpakaviongozi hawa wa ngazi za juu kupelekea taarifa za kujiuzulu kwao ghafla.
0 Comments "SAIDI MECK SADIKI NA VIGOGO WENGINE WAWILI WAACHIA NGAZI SERIKALINI "