Ya Rohoni! Nchi hii imebarikiwa kuwa na mito,maziwa,mabwawa,bahari na rasilimali za gesi asilia na mafuta karibu ktk kila kona na pembe zake! Miaka inakwenda kila hali ya huduma za mashirika haya Mawili inazidi kuzorota Siku zote!
Upatatikanaji wa huduma hizi umekuwa wa kusuasua na zenye matatizo yasiotibika wala kuzuilika! Ktk umeme tulifikiri kupatikana kwa gesi itakuwa suluhisho kupata umeme wa uhakika na kuepusha watu,ofisi,viwanda kukosa huduma hii muhimu kabisa!
Kwa nyakati tulizo nazo shughuli nyingi zinategemea uwepo wa huduma hizi mbili za maji na umeme.
Ajabu ya mungu hata ile miji iliyopo ktk maeneo ya rasilimali ya maji kama maziwa Victoria,Tanganyika,nyasa,manyara,rukwa bado watu wanateseka kwa mamlaka husika kushindwa kuwahudumia wateja wao kiwango sahihi na kila Siku kubaki kutoa visingizio lukuki kama ubovu wa mashine,ukosefu wa vifaa licha ya watu kulipa kulipa Ankara zao kwa wakati.
Wale wenzangu na Mimi watu wa nishati ya umeme hali ndio mbaya maradufu licha ya watu Wengi kulipa Ankara zao kwa wakati ukiachana na hao wakubwa manao waonea aibu!
Mbaya zaidi umeme unakatwa hata Mara 10 kwa kutwa au siku nzima bila taarifa rasmi tena ktk maeneo ya walalahoi ambayo Wengi wamefungiwa machine za kulipa kwanza kabla ya kutumia! Lakini kwa wale wasiolipa umeme iko kwa SAA 24/7,hii ni ajabu kila Siku nyinyi ni visingizio vya mashine fulani mbovu,huwa nakaa na kujiuliza pesa zinazolipwa huwa zinafanya kazi ipi? Na kushindikana kununua hizo mashine na vifaa?
Kiukweli huduma hizi za maji na umeme zimekuwa kero kubwa ktk uapatikanaji wake! Mbaya zaidi hata mteja anapohitaji kuunganishiwa huduma hizi inakuwa kama adhabu kubwa ya miaka kadhaa na kubembeleza!
Kifupi huduma zinatolewa chini ya kiwango na sio za kuaminika kabisa na usambazaji wenu wa huduma hizi umezidiwa na kasi ya wateja,nachojua Mimi ni vizuri bidhaa zikawa nyingi kiasi wateja wote wakapata na zikibaki utauza kesho kuliko kuwa na chache wateja wakaja wakakosa.
Kwakweli nyinyi pesa hamzitaki wenyewe Ila watu wanahitaji huduma hizi ni wote,na kwa njia hii ndoto Ya JPM Tanzania ya viwanda mnaiangusha kabisa,kwani viwanda vingi vinahitaji uwepo wa maji na umeme wa uhakika kwa japo 85% ili vinafanikishe.
Wengi wetu kutokana na umeme huu hakuna kazi au kitu unachoweza kukifanya kinachohusisha matumizi ya umeme au maji na ukawa na uhakika nacho kuwa utakimaliza salama bila kukatika kwa huduma hizi ghafla!
Mbaya zaidi huduma hizi zinaweza kukosekana Siku za mapumziko,sikukuu kwa kutwa nzima.
Mpaka hapa tulipofikia hatuelewi nini tatizo lenu? Sasa kuna umauhimu gani wa kupewa rasilimali hizi ktk nchi alafu zinashindwa kutusaidia?
Watanzania tujitahidi kuwa wazalendo mambo haya hata nchi kama Irani,misri,Saudi Arabia,Israel,Libya,morocco,Tunisia,Namibia,ambazo ni jangwa na wana vyanzo vichache vya maji Ila hawateseki kiasi hiki!
Wanatumia rasilimali hizo chache tu kujikwamua kiuchumi na kujiondolea matatizo mengi ktk maisha(mfano misri wao wanategemea mto Nile tu kama chanzo kikuu cha maji).
Tumechoka kuzungumzia hizi habari ambazo mataifa mengine walishaacha kuongelea zaidi ya miaka 200 sasa.



0 Comments "MASHIRIKA HAYA LINI HASA YATAFANYA KAZI ZAO JAPO KWA 70% TU?"