
Adam Kighoma Ali Malima aliyewahi kuwa naibu waziri wa wizara ya fedha wakati wa utawala wa serikali ya awamu ya nne iliyoongozwa chini ya Mh.Jakaya Mrisho Kikwete jana amekutana na maswahibu makubwa kama yaliyowahi kumkuta aliyekuwa waziri wa Michezo vijana na sanaa Mh.Nape Nnauye kwa kufyatuliwa risasi kadhaa hewani na wanaohisiwa ni makachero wa usalama wa taifa.
Adam Malima amekutana na sakata hilo akiwa eneo la masaki Dar es salaam katika mizunguko yake ya kawaida na dereva wake,kosa kubwa ni kupaki eneo lisilo ruhusiwa na hivyo kuwalazimisha watu wa action mart wenye mamalaka ya kuondoa magari yaliyopaki hovyo kutaka kunyanua gari hiyo pasipo na idhini ya dereva hivyo kulete purukushani kubwa kiasi cha kujaza watu ghafla ktk eneo hilo ili kshuhudia nini kinajili.

Askari hao wakiwa ktk majibizano na dereva kwa kumaka apeleke gari kituoni ndipo Bw.Adam malima alipotoka nje na kukuta mzozo huo ukiendelea baina ya dereva wake na askari hao w jeshi la polisi kuamaua kuingilia huku akijitambulisha kwa nyadhifa zake za awali,licha ya kufanya hivyo bado polisi walimtaka apeleke gari hiyo kituoni na yeye aliendelea kugoma hapo wananchi walikuwa pembeni waliamua kuzomea askari wakati wanataka kuondoka ndipo askari mmoja aliamua kushuka na kulazimisha gari iende yadi kwa kuingia ndai ya gari ya Adam malima.

Baada ya mda mchache tu askari mmoja alitoka na kuamua kufyatua risasi tatu hewani ikiwa ni ishara ya watu kutawanyika eneo hilo,lakini haikufua dafu hata hivyo ndipo askari walipoamua kumchukua Adam malima kinguvu akiwa na dereva wake na kuwaamuru kuingia ndani ya gari ya polisi na kuwapeleka kituo cha polisi na kulala huko mahabusu hadi leo walipofikishwa mahakama ya kisutu jijini Dar es salaam kujibu shitaka la kuzuia askari kufanya kazi yao ya halali.
0 Comments "ADAM MALIMA ASIMAMISHWA KIZIMBANI "