UINGEREZA WAHAHA KUJITOA UMOJA ULAYA:WAZIRI MKUU AITISHA UCHAGUZI MKUU TENA MWEZI WA SITA BAADA YA BUNGE LA WESTMINSTER KUPINGANA

Waziri mkuu wa uingereza Bi Teresa May ameistua dunia leo baada ya kutoa ujumbe mzito kutoka Bunge la House of Common juu ya majadiliano yanayoendelea kuhusu swala la uingereza kujitoa ktk umoja wa ulaya wakati wananchi walipopiga kura kipindi cha kiangazi mwaka jana ili kujua idadi ya wanaotaka na wasiotaka kuendelea umoja wa ulaya.

Hatimaye kura hizo wananchi wengi waliangukia kwa wengi wao kupiga kura ya ndio juu kujiondoa umoja wa ulaya,ila kumekuwa na upinzani mkubwa kwa watu waliopiga kura ya kubaki ktk umoja huo wakiwemo wengi kutoka scotland na kuleta mtafaruku mkubwa kiasi cha waziri mkuu wa scotland kutaka kujitenga na uingereza kwakuwa wao wengi hawajapiga kura ya kujiondoa bali kubaki.

Ndani ya wajumbe wa House of commons kama bunge pia wamekuwa wakipingana sana na kusababisha kufikia leo waziri mkuu huyu ambae hana mda mrefu toka kuingia kwake mwaka jana baada ya aliyekuwepo Donald Cameroon kujiuzulu kwakuwa aliapa endapo uingereza itapiga kura ya ndio kujiondoa umoja wa ulaya basi atajivua wadhifa huo.

Leo waziri mkuu kwa masikitiko aliwahutubia wananchi wa uingereza kupitia vyombo vya habari nkuwa waingereza wote mmepiga kura ya ndio kujitoa umoja ulaya lakini ndani ya bunge la westminster wao wanapingana hivyo kesho wabunge wote watapiga kura ya ndio u hapana ili kuwezesha kufanyikan kwa uchaguzi mkuu tena tarehe 8/6/2017.

Hali imekuw tata sana ndani ya uingereza kwa swala hili la kujiondoa au kubaki ndani ya umoja wa ulaya.

Matokeo ya ya kula za wabunge kesho ndio yatakayotoa ruhusa au kusitisha kufanyika kwa uchaguzi huo wa juni 8.



Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "UINGEREZA WAHAHA KUJITOA UMOJA ULAYA:WAZIRI MKUU AITISHA UCHAGUZI MKUU TENA MWEZI WA SITA BAADA YA BUNGE LA WESTMINSTER KUPINGANA"

Back To Top