
Toka kuingia kwa utawala mpya wa Donald Trump huko marerkani nchi hasimu za taifa hilo zimejikuta zikiingia ktk matata baada ya Rais huyu kufanya kweli na kuchukua hatua ngumu zaidi kwa mataifa au vikundi hivyo anavyoviita vya kigaidi licha ndani ya ahadi zake wakati wa kampeni aliahidi kuifanya marekni kuwa kubwa tena kwa kukuza uchumi wa viwanda,kukuza ajira na kuacha kuingiza nchi vitani kwani ni kuifanya nchi kutumia pesa nyingi kushughulikia mambo ya nje zaidi kuliko ndani.
Hivi karibuni jeshi la anga la marekani limepiga mama wa mabomu yote lijulikanalo kama MOAB (mother of all bombs) ktk milima ya afghanistan na kuua waasi wa IS 36 waliokuwa wamejifuicha ktk mapango yaliopo ktk milima hiyo.

Bomu hili la MOAB sio bomu la kinyuklia ila lina madhara makubwa pindi linapotumiwa linaweza kufanya milima mikubwa kuwa tambarare kabisa kutokana na nguvu zake. MOAB lenye uzito wa tani 11 haliwezi kutumiwa ila kwa ruhusa ya Rais wa nchi pekee.
Wiki iliyopita marekani walipiga mabomu 59 kutoka ktk meli zao za kivita kuelekeza kambi ya jeshi la anga la syria na sasa mareakani wanapeleka meli zao za kivita kuelekea ukanda wa Rasi ya korea kasklazini na korea wao wamesema wako Tayari kwa vita.
0 Comments "TRUMP HASHIKIKI SASA ADONDOSHA BOMU LA TANI 11 AFGHANISTAN"