MELI ZA KIVITA ZILIZOSHENI NDEGE NA SILAHA ZASOGEZWA KUELEKEA PENINSULA YA KOREA KASKAZINI

Jeshi la kimarekani limeamua kuanza kusogeza karibu zaidi meli na manowari zao za kivita eneo la penisula ya bahari ya pasifiki kueleke korea kaskazini kutokana na ubishi wa korea kaskazini kuendelea na itikadi zake za kutengeneza na kutumia silaha za kinyuklia na kuwatishia majirani zake kama japan na korea kusini wanaoungwa mkono na mataifa ya ulaya na marekani.

Meli hizi aina ya Carl Vinson zilizotengenezwa mwaka 1982 zina uwezo wa kubeba ndege za kivita 90 na watu wapatao 6062 na ina urefu upatao mita 1092 kuwezesha ndege kuruka na kutua zikiwa katikati ya bahari kuu bila tatizo.


Hatua hii ya marekani inawafanya watu kujiuliza maswali je hii inataka kuwa vita ya pili ya korea kiacha ile ya miakaya 1955? Rais mpya wa marekani Donald Trump amekuwa akionyesha ubabe wake kwa mataifa yote yaliyo ni mahasimu na maadui kwa kumiliki silaha za kinyulia na magaidi ambao wanasumbua ulimwengu.

Kwa hatua hii inaifanya korea kaskazini kujitaarisha kivita zaidi kwa kuendelea kurusha makombala yake ya majaribio.


Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "MELI ZA KIVITA ZILIZOSHENI NDEGE NA SILAHA ZASOGEZWA KUELEKEA PENINSULA YA KOREA KASKAZINI"

Back To Top