OPERESHENI YA KUONDOA WAFUGAJI HARAMU YASABABISHA MKUU WA WILAYA NGARA KUPOTEA MSITUNI KWA SAA 14

Mkuu wa wilaya Ngara Mkoani Kagera Bw.Godfrey Mweruka akiwa na maafisa wengine wa jeshi la polisi wamejikuta wakitangatanga msitu wa kimisi uliopo wilayani humo baada kuingia ndani ya msitu huo kwa kusudia la kusaka wahamiaji haramu ambao ni wafugaji kutoka nchi za rwanda na burundi.

Wafugaji hao ambao wameingia na kuvamia msitu huo wakiwa na mifugo yao mingi huku wakifanya na shughuli za kilimo.

Mkuu wa wilaya huyo akiwa na kundi la maafisa polisi wakiwa na magari kadhaa waliingia msituni humo na kujikuta wakipoteana kutokana na hali ya njia nyingi kufulika maji na matope kiasi ya gari nyingi kunasa hovyo.

Hata hivyo mkuu wa wilaya huyo na wenziwe walifanikiwa kurudi salama na kueleza kilichowakuta.

Wafugaji hao wanashukiliwa na jeshi la polisi kwa kuingia nchini pasipo na kibali,kuingiza na kuendesha shughuli za ufugaji na kilimo ndan ya hifadhi ya taifa.

Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "OPERESHENI YA KUONDOA WAFUGAJI HARAMU YASABABISHA MKUU WA WILAYA NGARA KUPOTEA MSITUNI KWA SAA 14"

Back To Top