JACOB ZUMA APIGWA MARUFUKU KUHUDHURIA MAZISHI YA AHMED KATHARADA

Mazishi ya aliyekuwa na mpingaji wa ubaguzi wa rangi nchini afrika kusini Bw.Ahmed Kathrada yamefanyika leo na huko afrika kusini huku Rais wa taifa la hilo kushindwa kuhudhuria mazishi hayo kutokana na waraka wa mwanaharakati huyo aliouacha kama wasia kwa familia yake.

Ahmed katharada aliacha wasia uliotaka siku ya mazishi yake kutozikwa kiserikali wala kutohudhuriwa na Rais Jacob Zuma kwakua alishamwandikia barua ya wazi juu yake kuwa anatakiwa kujiuzulu mara m,oja kwani amekiuka miiko na maadili ya chama tawala ANC kwa kukandamiza uhuru wa wananchi na kashfa za rushwa zilizokithiri ndani ya serikali yake hiyo.

Kumekuwa na mashinikizo mengi kutoka chama cha upinzani EFF kupitia kongozi wake Bw.Julius Malema kuitisha maandamano kumtsks  Zuma kujiudhulu bila mafanikio.

Kutokana na kashfa hizo ilimladhimu mkongwe huyo aliyetumikia kifungo cha miaka mingi ktk kisiwa cha robinson pamoja na Nelson Mandela kuandika barua huyo kumtaka Rais Zuma kujiuzulu haraka lakini juhudi hizo hazikuzaa matunda mpaka anafariki jana akiwa na umri wa miaka 87.




Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "JACOB ZUMA APIGWA MARUFUKU KUHUDHURIA MAZISHI YA AHMED KATHARADA"

Back To Top