MSUMBIJI YAWAFUKUZA WATANZANIA

Zaidi ya watanzania hamsini na nane (58) wamefukuzwa kwanguvu kutoka nchini msumbiji na kurudishwa hadi kijiji kilichopo mapakani mwa Tanzania na msumbiji kiitwacho (kilambo) na kutupwa hapo wakiwa hawajui nini cha kufanya.

Sakata hilo limetokea ghafla kuanzia juzi na kufanya na askari wa nchi hiyo ambao uenda kwenye nyumba wanazoishi watanzanianchini humo na kudai karatasi ya ruhusa ya kuishi humo maarafu (documento) na ikiwa huna basi ukubeba kinguvu na kukupandisha ktk magari yao na kuwapeleka hadi mpakani hapo na kuwwacha kwenye mataa wasiwe na cha kufanya.

Walipoulizwa kwanini wanazanin wanafanyiwa hivyo licha ya wao kuishi ktk nchio hiyo kwa muda mrefu kiasi cha kuoa,kuzaa na kumiliki mali na vyumba ktk nchi hiyo,waliabaki wakiwa hawana jibu zaidi ya kushangaa tu kwanini imekuwa hivyo kwani hakuna tatizo walilofanya  ktk nchi hiyo na wana mahusiano mazuri toka zamani na ikikumbukwa kuwa Tanzania waliwasaidia watu wa msumbiji ktk vita ya kujikomboa na wakoloni walowezi kireno mwaka 1975,na kupoteza wanajeshi wengi waliozikwa mkoani mtwara kijiji cha naliendele.

Ila alipoulizwa mwenyekiti wa serikali za mitaa wa kijiji cha kilambo kilichopo mpakani karibu na mto ruvuma alisema waowanahisi tatizo ni kuwa kuna mzungu mmoja toka nchi hiyo alifukuzwa kutoka mtwara mjini eneo mikindani anaejulikana kama (franco) hivyo yawezekana kisa kikawa ni hiko.

Watanzania hao waliofukuzwa wameletwa mtwara mjini ili kufanya utaratibu wa maongezi ili kujua tatizo na ikiwezekana kurekebisha kasoro hizo.


Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "MSUMBIJI YAWAFUKUZA WATANZANIA"

Back To Top