
Mtu huyo wa makamu aliingia ndani ya uwanja wa mpira wa Baseball uliopo jirani na viwanja hivyo vya jengo kongwe la Capitol hill ambapo baadhi ya maofisa walikuwa wakifanya michezo na mazoezi mbalimbali na kuamua kufyatua risasi hovyo na kuumiza zaidi ya watu watano 5 akiwemo mwanasheria maarufu wa baraza la congress Steve Scalise aliyeumia vibaya sana na kukimbizwa hosptali akiwa mahututi.

Pia polisi waliongeza kuwa inawezekana mtu huyu ana matatizo ya akili ndio maana aliamua kufanya hivyo na sio kitendo cha ugaidi kama wengi wanavyohisi.

0 Comments "MZEE WA MIAKA 66 AMWAGA RISASI MCHANA KWEUPE JIRANI NA JENGO LA BUNGE LA MAREKANI"